City Pages
City Pages ni gazeti la kila wiki la mbadala kwa magazet mengine.Gazeti hilo ni la eneo la Minneapolis-St.Paul. Gazet hili hushirikisha habari, filamu, maigizo na maoni kuhusu mikahawa, na maoni kuhusu muziki. Linachapishwa katika mfumo wa gazeti la porojo na linauzwa kila Jumatano. Gazeti hili lililochapishwa na Village Voice Media,ni kampuni linalochapisha magazeti 16 lililo na makao yake Phoenix,Arizona.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Tarehe 1 Agosti 1979, wachapishaji Tom Bartel na Kristin Henning walichapisha jarida la kila mwezi lilioitwa Sweet Potato lilihusika sana na sekta ya muziki katika eneo la Twin Cities. Toleo la kwanza la bendi la pop liloitwa The Cars kwenye ukurasa wa kwanza. Mnamo mwezi wa Oktoba 1980, Sweet Potato ikaanza kuchapishwa baada ya wiki mbili. Tarehe 3 Desemba 1981, gazeti likaanza kuchapishwa kila wiki na kuitwa City Pages. City Pages ilishindana na gazeti la The Twin Cities Reader mpaka mwaka wa 1997 ambapo kampuni ya uchapishaji ya Stern Publishing ilinunua City Pages mnamo Machi na ikanunua The Twin Cities Reader siku iliyofuata. Bartel na Henning walitoka City Pages katika mwaka wa 1997. Kaka wa Tom Bartel,Mark,akaajiriwa kama mchapishaji baada ya Bartel na Henning kuondoka. City Pages ilikuwa mojawapo ya magazeti ya kila wiki yaliyomilikiwa na Stern, Village Voice ikiwa moja yao. Tarehe 24 Oktoba 2005, New Times Media ilitangaza mpango mpya wa kununua Village Voice Media, ikiunda mnyororo wa magazeti 17 (hivi sasa 16) ya bure yanayochapishwa kila wiki kote nchini na kuwa na usambazaji wa magazeti(ya kila wiki) milioni 1.8. Hivyo basi waliendesha robo ya usambazaji wa magazeti ya kila wiki nchini Marekani. Baada ya kukamilika kwa mpango huo, New Times ilichukua jina la Village Voice Media.
Usambazaji wa City Pages ni 25.4% katika soko la Twin Cities.Nakala 100,000 zikichapishwa kila wiki kwa wasomaji wa 329,800. Takwimu ya kijinsia kuhusu wasomaji: Wanaume :52.9% (nakala ya kuchapishwa) 49% (kwenye tovuti ya gazeti),Wanawake: 47.1% (nakala ya kuchapishwa) 51% (katika tovuti ya gazeti).
Mhariri wa tovuti, Jeff Shaw,mwandishi wa makala ya chakula,Dara Moskowitz Grumdahl na waandishi wengine,Jonathan Kaminsky na Jeff Severns Guntzel waliondoka katika mwaka wa 2008.
Angalia pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- City Pages, LLC. ^ "Advertising Information".
- Schmelzer, Paul (10 Septemba 2008). The Minnesota Independent. "More altweekly exits: Shaw, Kaminsky to depart from City Pages"